Robert LutherKarl Theodor Robert Luther (Świdnica, 16 Aprili 1822 - Düsseldorf, 15 Februari 1900) alikuwa mtaalamu wa nyota (mwanaastronomia) kutoka nchini Ujerumani. Alifanya kazi katika Bilk Observatory huko Düsseldorf, Ujerumani, alitafuta asteroidi na kuzigundua 24 kati ya mwaka 1852 na 1890. Ni mshindi wa tuzo ya Lalande mara saba. WasifuRobert Luther alizaliwa 16 Aprili 1822 na wazazi wake Luther na Wilhelmine von Ende. Alisoma nyumbani na baada ya hapo katika shule ya secondari ya eneo hilohilo. Mnamo 1841 alihamia chuo cha Breslau ambapo alisoma hadi 1843. Mnamo 1843 Luther alihamia Berlin kusomea masomo ya unajimu. Alikuwa mwanafunzi wa Johann Franz Encke na akamsaidia katika hesabu zake za astronomia. Mnamo 1850 alikua mchunguzi wa pili katika chuo. Mnamo 1851, Franz Brünnow alimwalika Luther kwenye Düsseldorf-Bilk Observatory kuwa mkurugenzi wa uchunguzi baada ya kustaafu kwake. Luther alimuoa Caroline na walikuwa na mtoto mmoja wa kiume, William. Luther alikufa mnamo 1900 kwa ugonjwa mfupi huko Düsseldorf. UgunduziLuther aligundua nyota 24 kati ya mwaka 1852 na 1890. Ugunduzi wake sasa unajulikana kwa kuwa na sifa zisizo za kawaida: Asteroidi zenye sifa sawa, Antiope 90 na glauke inayozunguka polepole sana. Aligundua asteroidi 25 zifuatazo:
Heshima na tuzoAlitunukiwa tuzo ya Lalande mara saba, mnamo miaka ya 1852, 1853, 1854, 1855, 1859, 1860 na 1861 na Royal Astronomical society. Mnamo 1869, alikabidhiwa medali ya ukumbusho ya unajimu.
Information related to Robert Luther |
Portal di Ensiklopedia Dunia