A Tribe Called Quest
A Tribe Called Quest ni kundi la muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Kundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1985, [1] na linaunganishwa na rapa/mtayarishaji Q-Tip, rapa Phife Dawg aka Phife Diggy (Malik Taylor), na DJ/mtayarishaji Ali Shaheed Muhammad. Mwanachama wa nne, rapa Jarobi White, aliondoka kundini baada ya kutoa albamu yao ya kwanza na kurudi tena kundini mnamo mwaka wa 1991. Akiwa na De La Soul, kundi lilikuwa sehemu ya kati ya Native Tongues Posse, na wamefurahia mafanikio ya pamoja hasa baada ya kila kundi kuwa kimpango wake kwa mkusanyiko huo. Uvumbuzi wao unayeyusha hip hop na jazz umefanya uwe na mgongano mkubwa katika muziki wa hip hop, umesaidia kupanua wigo wa sanaa ya utayarishaji wa muziki wa hip hop. Nyimbo zao nyingi kama vile "Bonita Applebum", "Can I Kick It?", "I Left My Wallet in El Segundo", "Scenario", "Check the Rhime", "Jazz (We've Got)", "Award Tour" na "Electric Relaxation" hutazamiwa kama classic na jumuiya za hip hop. Wametoa albamu tano kati ya 1990 na 1998. LP zao za kwanza zilikuwa maarufu mno, lakini kundi lilivunjika mnamo mwaka wa 1998. Mnamo 2006, kundi limeungana tena na kufanya ziara kadha wa kadha nchini Marekani, na kutoa ahadi ya kwamba watatoa albamu baada ya kufanya kazi katika mastudio kadha wa kadha. Kundi hutazamiwa kama miongoni mwa makundi wavumbuzi wa alternative hip hop, kwa kusaidia kuweka njia ya kwa wasanii wapya wa hip hop.[2] John Bush wa Allmusic kawaita "kundi la rap lenye akili zaidi la miaka 1990,"[3] wakati wahariri wa About.com wamewapa nafasi ya #4 kwenye orodha yao "Makundi 25 ya Rap ya Muda Wote."[4] Mwaka wa 2005, A Tribe Called Quest wamepata Tuzo ya Special Achievement Award kwenye Billboard R&B Hip-Hop Awards huko mjini Atlanta.[5] Mwaka wa 2007, kundi pia lilipewa heshima yake kwenye 4th VH1 Hip Hop Honors. DiscografiaAlbamu
Kompilesheni albamu
Marejeo
Viungo vya NjeInformation related to A Tribe Called Quest |
Portal di Ensiklopedia Dunia