Yohane Thanh Van DinhYohane Thanh Van Dinh (1796-1840) pamoja na katekista mwenzake Petro Nguyen Van Hieu (1783-1840) na padri Paulo Pham Khac Khoan walikaa kwanza gerezani miaka 3 wakiteswa ili wakane imani yao ya Kikristo, hatimaye wakakatwa vichwa vyao chini ya kaisari Minh Mang. Ni kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886). Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116. Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988. Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe ni tarehe 28 Aprili[1]. Tazama pia
TanbihiMarejeo
Viungo vya nje
Information related to Yohane Thanh Van Dinh |
Portal di Ensiklopedia Dunia