Mkoa wa Arusha
Mkoa wa Arusha ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 23000, na ni wa pili kwa utajiri nchini. Wakazi ni 2,356,255[2]. EneoEneo lake ni km za mraba 34,526 zikiwemo km² 707 za maji ya ndani.[3]. Umepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani, kufuatana na mwendo wa saa, ni: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara. Wilaya zake ni Monduli, Longido, Meru, Arusha Vijijini, Arusha Mjini, Ngorongoro na Karatu. Makao makuu yapo Arusha mjini. Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai (m 2,878) ni volkeno hai bado, na mlima Meru ni volkeno iliyolala tangu mwaka 1910. Mvua hunyesha kati ya milimita 1,800 kwa mwaka mlimani Arusha hadi mm 508 kwa mwaka katika maeneo makavu. UchumiMkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Tarangire ziko karibu. Barabara ya lami Dar es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi. Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti. Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea. Kati ya wakazi asili wa mkoa ndio Waarusha, Wameru, Wairaqw na Wamasai. Majimbo ya bungeWakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
Tazama piaTanbihi
Viungo vya nje
Information related to Mkoa wa Arusha |
Portal di Ensiklopedia Dunia