Lady Jay Dee
Maisha ya awaliJudith Wambura alizaliwa na Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake. Alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba. Alianzia kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi. Baada ya kumaliza shule, Lady Jaydee aliwahi kufanya kazi Clouds FM kabla ya kuamua kujiingiza kwenye masuala ya muziki hapo mnamo miaka ya 2000.[2] Shughuli za muzikiAlianza kujibebea heshima katika medani ya muziki kunako mwaka wa 2000 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Machozi" na kutoa single kadhaa kutoka katika albamu hiyo na kumfanya kuwa mwanamama wa kwanza katika bongo flava kwa kutumia gharama kubwa ya ujenzi wa albamu katika historia ya muziki wa kizazi kipya. Lady Jay Dee ni msanii mwenye kumiliki studio yake mwenyewe ya kurekodia. Studio inakwenda kwa jina la Jag Records. Jay Dee, alishawahi kuchaguliwa kuwa Mwanamuziki Bora wa Kike wa Tanzania kwa muziki wa R&B mnamo 2002, na kutumbuiza katika Kora All Africa Designers Competition, na kutuzwa "Albamu Bora ya R&B" katika Tuzo za Muziki Tanzania kunako tar. 6 Agosti 2004. Kunako mwezi wa Julai 2005, ameshinda tuzo ya "video bora ya msanii wa kike kwa Afrika Kusini". MuzikiAlbamu zakeJay Dee, ametoa albamu saba za muziki:
Marejeo
Viungo vya Nje
Information related to Lady Jay Dee |
Portal di Ensiklopedia Dunia