JamiiJamii ni istilahi inayoelezea uwepo wa pamoja wa mwanadamu (kwa pamoja, inataja jumla ya mitandao ya kijamii na nguvu ya mitandao yake) ama ni jumuiya ya watu wanaoishi pamoja kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni walizojiwekea kwa lengo maalum la kulinda na kukuza tamaduni zao za kimila. Haitaji kila kitu ambacho mtu anafikiria kuwa nacho au hana, bali yale ya mambo ambayo kila mtu anayetenda kwa dhumuni maalumu. Jamii ni watu wanaokaa pamoja na kushirikiana kwa mambo mbalimbali, kwa mfano masuala ya afya, elimu na ulinzi: mambo hayo yanapowakutanisha watu hujenga kitu kinachoitwa jamii, jamii hujenga umoja na upendo baina ya watu husika. Jamii bora inahitaji watu wenye upendo: watu wakipendana huweza kuishi na kujenga jamii bora, hivyo ni vyema watu wa sehemu husika wapendane ili waweze kujenga jamii ya namna hiyo.
Information related to Jamii |
Portal di Ensiklopedia Dunia