Isaac Asimov
Isaac Asimov (mnamo 2 Januari 1920 - 6 Aprili 1992) alikuwa mwandishi wa bunilizi ya kisayansi nchini Marekani. Alikuwa pia mtaalamu wa biokemia mwenye PhD kutoka MaishaAsimov alizaliwa huko Petrovichi, Smolensk, Urusi katika familia ya Kiyahudi. Tarehe ya kuzaliwa haijulikani, ilitokea kati ya 4 Oktoba 1919 na 2 Januari 1920. Alisheherekea sikukuu yake kwenye 2 Januari. Wazazi walihama Marekani pamoja naye alipokuwa na umri wa miaka 3. Alijifunza lugha za Kiyiddish na Kiingereza tangu utotoni. Alisoma kemia kwenye Chuo Kikuu cha Columbia akahitimu shahada ya uzamili kwenye mwaka 1941 akaendelea kupokea digrii ya uzamivu (PhD) mnamo 1948. Wakati huohuo aliandika pia masimulizi na vitabu. Tangu 1951 alikuwa profesa kwenye Chuo Kikuu cha Boston ilhali aliendelea kuandika. Baada ya mafanikio ya kitabu chake The Naked Sun (1957) aliacha kazi ya kisayansi akaendelea kutunga vitabu vyake. Aliandika vitabu vingi, hasa masimulizi na riwaya juu ya ustaarabu ujao ambako watu huishi pamoja na roboti yaani mashine zenye uwezo wa kufikiri zinazopewa maumbile ya kufanana na binadamu. Asimov alitunga pia vitabu vinavyoeleza sayansi kwa watu waskio wataalamu alikuwa mshauri wa kisayansi kwa filamu za Star Trek zilizotengenezwa kwa runinga. MaandishiVitabu vya Asimov's vilivyokuwa mashuhuri zaidi vilikuwa vitabu vya mfululizo wa Foundation series. Aliandika pia Galactic Empire na Robot Series. Kwa jumla alitunga au alihariri zaidi ya vitabu 500 akaandika barua 90,000 letters. Pamoja na bunilizi ya kisayansi aliandika pia kuhusu sayansi yenyewe, historia, Biblia, fasihi na Maandishi mengi ya mapema ya Asimov yalikuwa hadithi fupi zilizochapishwa katika majarida na daftari za hadithi za bei rahisi. Miaka baadaye, yalikusanywa na kuchapishwa tena kama makusanyo. Mikusanyiko inayojulikana ni pamoja na I, Robot, The Rest of the Robots, Earth is Room Enough na The Early Asimov. Orodha ya AsimovAsimov alitunga orodha ya vitabu vyake 15, akishauri visomwe kwa utaratibu huu:
1-5 ni vitabu vya 'Roboti'; 6-8 ni vitabu vya 'Galacticos Empire'; 9-15 ni vitabu vya mfululizo wa Foundation . [1] Riwaya za Asimov zimeathiri bunilizi ya kiayansi kwenye runinga na sinema. Hasa 'Three Laws of Robotics' (kanuni tatu za uroboti) zilichangia kwenye majadiliano ya kimataifa kuhusu teknolojia hiyo.
ImaniIngawa alizaliwa katika familia ya Kiyahudi, Asimov alijiita kafiri anayekana Mungu:
KifoAlipofanyiwa upasuaji wa moyo mnamo 1983, alipokea damu iliyoambukizwa VVU. Alipata UKIMWI, akafa kutokana na athari za hali ya kiafya mnamo 1992.[3] Marejeo
Viungo vya NjeWikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Information related to Isaac Asimov |
Portal di Ensiklopedia Dunia