User:DARIO MARIBA

HISTORIA YA WAKURYA TANGU MWAKA 1200.

Kitabu cha ukoo wa Wakurya  ambao wanamilango mingi iliyotokana na vijana wa kiume wa Mzee Mkurya. Tuanze na“Wairege  waliozaliwa naMwirege” mwana wa Gurani. Gurani mwana wa mkurya. Mkurya mwana wa Mogango na Magango mwana wa Monto. Na ndugu zake Mogango ni Range Magaiwa na Mtatiro, ambao wao walitokea katika kundi/jamii ya Kibantu na wabantu walitokea Misri ambao wao walitokea Mesopotamia huko Iraq. Na baada ya kuingia Misri walijitenga kutoka kwa waarabu wakaenda Mandara huko Camerooni ambako ndiko chimbuko la wabantu. Lakini baadae jamii hiyo ya kibantu iligawanyika na kutengana,  jamii nyingine ilirudi Misri wakati wa utawala wa Farao mfalme wa Misri, ambako hiyo jamii iliungana na wana wa Israel kutumikia utumwa.

Kihistoria hapo ndipo walitokea mababu wa Kikurya,tangu wakati huo wakurya ndipo walipopata miiko ya Kiisraeli, kama vile siku ya saba na tohara. Ingawa wakati huo hakukuwa na jina la “WAKURYA” Baada ya kutoka utumwani Misri walikwenda Ethiopia na kukaa huko kwa muda mrefu, na jamii nyingine zikatangulia kuingia nchi za Afrika Mashariki, jamii ya Wakurya ilifuatiliwa na Waarabu hadi kupigana kwa sababu ya ukataa utumwa, lakini Waarabu walitumia silaha kali yenye risasi iliyoitwa (MRONDO) silaha hiyo ndiyo Waarabu walitumia kuwaondoa kabisa Wakurya kutoka Ethiopia.

Baada ya vita hiyo, Wakurya  waliondoka na kuvuka mto Naili hadi Uganda sehemu za Sibuli Nyairongo na Mgini, huko Uganda Wakurya walikutana na jamii zingine ambazo zilikuwa zimetangulia kuingia huko kutoka sehemu mbalimbali walizokaa wabantu. Hapo Uganda walikaa sana, jamii walizokutana nazo ni Waluo, Watariki, Wamasai, na jamii zingine zilizoingilia mlima Elgoni kimya kimya. Jamii hizo baadae ziliondoka kutoka Uganda na kuingia mwambao wa  bahari ya Hindi. Kwa hiyo historia inaonyesha wazi kwamba Wakurya walitokea Iraq wakaingia Misri Comeroon Ethiopia, Uganda, Congo, Brazavili.

KUPATIKANA KWA WAKURYA:-

Jamii ya Wakurya ni kubwa sana ina historia ndefu. Kupatikana kwa Wakurya, ni kutokana  na jamii iliyoanzishwa na mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la  MONTO (MTU). Yeye alijaliwa kupata watoto ambao ndio mababu wa Wakurya. Monto alimzaa Mogango, Range na Magaiwa, wakiwa huko Uganda ambapo baadaye jamii hizo zilitengana wakati wa kuingia Tanzania/Tanganyika, Mogango na jamii yake wao walienda Congo Brazil. Lakini  Range yeye na jamii yake pamoja na Wamasai walihamia sehemu za Busia huko Kenya na hatimaye waliingia Kondoa Irangi yaani Kondoa . Jamii ya Mogango wao waliingilia Kigoma hadi Uvinza kwenye maji ya chumvi wakanywesha mifugo yao huko. Baadaye walitoka Kigoma wakainigia Mwanza huko walipofika wakatazama yale maji  ya ZiwaVictoria wakapaita (“INYANCHA) yaani ziwa tena huko Mwanza waliondoka baadaye ingawa hawakutaka.  Watu walipopata habari ya kuwa ndugu zao wapo sehemu za Kondoa walikwenda kuwatafuta ili wawe jamii kubwa.  Hili ndilo lengo lao la kuingia Kondoa na wakaishi huko na hadi sasa kuna mlima wa Wakurya uitwao Ngicharu” ambapo hapo ndipo alipozaliwa Mkurya,  ndugu yake ni Mugusuhi. Wao walizaliwa wawili na mzee Mogango. Kwa hiyo chimbuko la Wakurya ni Kondoa mlima Ngicharu, watu hao waliishi huko Kondoa muda mrefu, mpaka wao wakapata jamii kubwa ambayo ndiyo inayoitwa Wakurya.

Baada ya kuishi Kondoa, waliondoka kwenda sehemu za Goga wakati huo jamii ya Wakurya iliongozwa na nabii ambaye yeye alikuwa anatoa unabii kuonyesha dira ya sehemu ambazo watakwenda kumiliki. Basi wakaingia  Mogango baada ya kuinigia, ndipo walipozaliwa watoto wote wa Mkurya, Mkurya alioa mke jina lake Gati Ogete yeye ndiye mama wa kikurya huyu mama alijaliwa kupata vijana sita wa kiume na hapo ndipo lugha ya Kikurya ilizungumzwa rasmi hadi leo kwa sehemu za (Goga) ndipo kuna eneo linaloitwa Mogango ambako lilipatikana jina na lugha ya kikurya kwa maana nyakati zote za jamii hiyo ilikuwa ya kuhama hama..Kwa hiyo huko Mogango ndipo jamii yote ya kikurya ilitengeneza sera ya jamii hadi leo. Mzee Mkurya na mkewe Gati Ogete walijaliwa kupata vijana sita ambao ni:

Nyabasi Omkurya,

Gurani Omkurya,

Gisiri Omkurya,

Mosoba Omkurya,

Mkira Omkurya,

Msembete Omkurya.

Sehemu hiyo ina historia ya watoto wote wa Mkurya walikulia huko Mogango pamoja na jamii ya Mgusuhi. Baadaye jamii ya Mgusuhi ndiyo walitokea Wangorweme  na Waisenye,  wao walibaki katika Wilaya ya Serengeti na Bunda. Historia inaonyesha kuwa huko Mogango ndipo hata majina mengi ya wanyama na tohara za Wakurya na Wamasai  waliondoka kutoka Kondoa. Jamii hiyo Wamasai ilijulikana Punda milia na Ikiwere Nyumbu kana kwamba jamii ya mwikwabe hadi leo Waisraeli wanaitwa Waikwabe” kwa kikurya jamii ambayo  baadaye ilikuwa ni adui wa kikurya hadi leo.Majina mengi ambayo Wakurya wanatumia chanzo chake ni huko Mogango, majina mengi yamewakilisha wanyama kama vile.

Eng’ombe Ng’ombe

Imburi Mbuzi

Iring’ondi Kondoo

Inchungu Tembo

Inchage Punda milia

Ikewere` Nyumbu

Esagati Nyamera

Endwe Simba

Engwe Chui

Engoge Nyani

Egekondo Tumbuli

Egekene Komba

Inchoka Nyoka

Irisambo Shetani

Ichingoko Kuku

Ibinyuni Ndege

Isuma Swala

Inungu Mbuni

Ikinume Digi Digi

Egetocho Sungura

Amarwa Pombe

Obosara Togwa

Ubukima Ugali

Ikirunguri Uji

Amahemba Mtama

Ichaga Bangi

Eng’era Mbogo

Ihuburi Kifaru

Amabere Maziwa ya ng’ombe

Emete Miti

Omoroo Moto

MAJINA YA MIEZI

Kinyariri. January.

Itabarari. February.

Matui. March.

Kimwamu. April.

Kerapu. May.

Iheta.           June.

Mapeho/Pigembe.  July.

Nyansahi. August.

Ikurya. September.

Nyandemera . October.

Itirya ya mpere. November.

Itirya ya kapere. December.

HUU NI MPANGILIO WA UMRI WA RIKA KWA KABILA LA WAKURYA.

Omogaka ni mzee mwenye umri kuanzia miaka 50.

Umukungu ni mwanamke wa miaka zaidi ya 5o.

Omosacha ni mwanaume

Omogaikoro ni mwanamke

Umwiseke ni binti zaidi ya miaka 18.

Umumura kijana ambaye haja oowa ila zaidi ya 18

Sokoro           babu mwenye miaka zidi ya 60

Goko bibi mwenye miaka zaidi ya 50

Mulieha kijana mwenye miaka chini ya 16.

Mosagane binti mwenye umri chini ya 14.

Omona mtoto chini ya miaka 14.

Omosabati mama aliye olewa tayari.

Kwa hiyo huko mogango kuna chanzo cha majina ya watu kuitwa kulingana na kuzaliwa kwake. Majina yaliyo tumika mengi yalikuwa na msimu wao kulingana na nyakati maalum. Ndiyo maana majina mengi ya kikurya yana fanana kama vile Chacha, Mwita, Marwa. Upande wa wanaume na upande wa wanawake ni Bhoke, Rhobi na Ghati. Majina haya ni maalum kwa watoto wa kwanza kuzaliwa kulingana na jinsi ya mtoto, ila mtoto wa jinsi yeyote anaweza kuitwa jina lolote kati ya hayo sita kutokana na kumbukumbu za uzao wa baba na mama wa mtoto aliyezaliwa, hii ni kwa ajili ya kumuenzi  marehemu uliyeitwa kwa jina lake. Pia majina hayo yalitokana na matukio na yakati.

KUGAWANYA MAJINA YA MATUNDA YA MITI PORI.

Walikuwa wana angalia matunda yanayoweza kuliwa na binadamu yasiyo na sumu. Matunda hayo yaliwasaidia wakati wa njaa yalitumika kama chakula. Matunda hayo ni kama vile;

Ichinkarakara

Ichimange

Ubunyabotati

Ichinkomori

Ichihuru

Obosangora

Emerogo

Ibinguti

Hayo ndiyo matunda waliyo kula huko mogango wakati wa dhiki ya chakula. Wakati huo wakuryra walilima mazao ya mtama aina ya ekomba, na mbegu yake waliitoa Kondoa. Walilima nazi, viazi vitamu aina ya nyoga na pamoja na ulezi aina ya Isabara egesorekwe tena jamii hiyo ilipata mali  kwa njia ya urimbo na ulindi kwa kupekecha vijiti viwili hadi kipate moto tena watu kama wazee wao walitunza moto kwa kuweka jikoni magogo ya miti ambao hutunza moto kwa muda mrefu. Miti walitengeneza kwa ajili ya kutunza moto ni emerama na ememange hali hiyo iliendelea kwa karne nyingi zilizopita, kwa maana mambo hayo yote yalifanyikia huko Mogango. Kwa hiyo wakurya wanaitwa Kurya Omogango. Maana mwanzo wao ni MOGANGO.

KUGAWANYIKA KWA WAKURYA:-

Baada ya jamii hiyo ya Wakurya kukaa Mogango, kwa muda mrefu kabla ya kutengana. Walitengana na jamii ya Mugusuhi, waliokwenda Ikorongo, wengine Isaryo na wengine na waliogawanyika ni:-

Wanyiramba

Wakira

Wasembete

Wairige

Wamasoba

Wasiri

Watimbaru.

IHUKE: YAMORARYO.

Hapo ndiyo  iliwatawanya  Wakurya wote hadi leo, mtu aliyeonekana mara moja huko Mogango, Alikutana na NYOKA mwenye vichwa vinane, tangia wakati huo ndipo wakurya walipata AMAKORA ANANEI (8), kama vile vichwa vya nyoka VINANE.  Watoto waliozaliwa wakati huo  waliitwa APASAHE, ambao ndio ilikora la kwanza, waliofuata waliitwa APACHUMA lilikuwa ilikora lapili, Tangu wakati huo wakapata vizazi vinne vinne kutoka kwa apasahe na apachuma, yaani amakora(vizazi) ambayo mpaka leo yapo na yanaendelea. Vizazi hivyo viliifanya jamii ya Kikurya kuwa na utaratibu wa kuoa. Tena wakurya walikuwa mtu akifa kama ameacha mke lazima jamii yake indelezwe na ndugu zake ili awe na jamii.

AMAKORA (8)

Amakora haya manane yaliwekwa kwa muundo maalumu, ili kuepusha kizazi cha jamii moja kuoana wenyewe kwa wenyewe.

HIVI NI VIZAZI VINNE VINNE VYA JAMII ZA APASAHE NA APACHUMA.

KIZAZI CHA MONYASAHE KINAZAANA KAMA IFUATAVYO.

Apasahe wakawazaa Apanyampuriti,

Apanyampuriti wakawazaa Apagamunyeri,

Apagamunyeri wakawazaa Apamaina,

Apamaina wakawazaa Apasahe katika mzunguko mwingine/wapili.

KIZAZI CHA MONYACHUMAKINAZAANA KAMA IFUATAVYO.

Apamairape wakawazaa Apagini,

Apagini wakawazaa Apanyangi,

Apanyangi wakawazaa Apachuma,

Apachuma wakawazaa Apamairape katika mzunguko mwingine/wapili.

Kwa ujumla hivi vizazi vya MONYASAHE na MONYACHUMA hawakuwa na miiko ya kuoana. Miiko ilikuwa kwa kizazi kimoja, hasa kama mvulana atamuoa msichana ambaye ni mtoto wa IRIKORA la baba yake, pia mwanamume hakuruhusiwa kabisa kuoa msichana mwenye undugu wa karibu, au mtoto wa rika lake na  muoaji.

MWIREGE – OGURANI NA JAMII YAKE NI CHANZO CHA WAIREGE:-

Kitabu cha ukoo wa Wairege ni Mwirege mtoto wa Gurani, na Gurani mtoto wa Mkurya na Mkurya ni baba wa Wakurya na babu yao ni MOGANGO. Mwirege alizaliwa mtoto wa pekee wa kiume wa Gurani, na ndiye aliyetambikia ile nyoka mwenye vichwa vinane, na yeye alijaliwa kuwa na jamii kubwa kuliko wengine. Basi Mwirege alimuoa Nyamakora kutoka kwa jamii ya Mugusuhi. Mke huyo alijaliwa watoto wawili wa kiume ambao ni:-

NYAIRO OMWIREGE

NYASUNCHE OMWIREGE

Hao ndio watoto wa Mwirege Ogurani ambaye alikuwa mjukuu wa mwenye vijana hao walio oa kila mtu na mke wake ila Nyairo yeye aliooa wake wane na Nyasunsye alioa mke mmoja.

NYAIRO NA WAKE ZAKE:-

Mtu huyu yeye alijaliwa kuoa wake wangi na ndio maana wakurya Wairege wao huoa wake wengi kwa sababu ya huyu Nyairo.

MKE WA KWANZA WA NYAIRO;-

Nyairo alioa mke wake wa kwnza kutoka kwa Waisenye jina lake aliitwa GASEMBE ambaye alimzaa SIYEE na MAIRI. SIYEE alimzaa OBOGO na OBOGO alimzaa MUGINI na MUGINI alimzaa TUGARA na MWERA. Na MAIRI yeye alimzaa WANGESE ambaye alioa  BHOKE OSIMBORI aliyemzaa GASSAYA na GASSAYA alimzaa CHACHA na hiyo ndiyo  familia ya mke wa kwanza wa NYAIRO.

MKE WA PILI WA NYAIRO;-

Nyairo alioa mke mwingine jina lake Malale kutoka jamii watimburu ambaye yeye aliwazaa wankaba na Mongohe. Wankaba alimzaa Nyanwe , nyangw alimzaa Kivumbe ambaye alipanda mbegu ya nyama shambani. Mongohe alimzaa Marwa. Hiyo ndio familia ya mke wa lpili wa Nyairo.

MKE WA TATU WA NYAIRO:-

Nyairo alijitwalia mwanamke jina lake Nyamwamu, alikuwa na watoto  wawili wa kwanza alikuwa ni Kigueli na Pili. Hivyo mwanamke alizaa watoto wengine baada ya kuolewa na Nyairo watoto hao ni:-

WAMBURA

SAGIRE

RIMIRAMA

LAWE

Na baada ya kuwazaa watoto alipata watoto sita vijana hao wate walizaliwa huko Mugango.

MKE WA NNE WA NYAIRO”-

Nyairo alioa mke mwingine  jina lake aliitwa Masoba., aliyeolewa kutoka kwa nyaibara. Mke huyo alimzalia Nyairo watoto wa kiume alimzaa Mwita na Mwita alimzaa Habura. Gibeche Mohere mama aliitwa Omahe  kwa hiyo baadaye waliitwa Monyomahe kazi hiyo yote ilifanyikia Magango.

Hao ndio wake wa Nyairo mwana wa Mwirege mwana wa Gurani mwana wa mkurya mwana wa Mogango mwana wa Monto na Monto ni adam.

NYASUNJYE NA FAMILIA YAKE:-

Mtu huyu alioa mke jina lake Rhobi kutoka rolia msembete. Yeye nddiye alimzaa Giehere kijana huyo alizaliwa yeye pekee wa Nyasurye. Mambo haya yote yalifanyikia huko Mogango tena vizazi hivyo ndivyo walimotokea waanzilishi wa amakora tena huo ndio uzao wa MIREGE OGIRANI.

WAIREGE KUONDOKA MOGANGO NA KUINGIA GUCHINDAMA:-

Jamii ya wairege baada ya kugawanywa na yule nyoka wa vichwa vinane aliyeitwa IHUKE ya Nyamoraryo  Wairege wao walihamia sehemu ya molo Guilindama

ng’ambo yam to Mara. Lakini katika sehemu hiyo chakula kiliwapa shida ingawa mboga zilikuwa nyingi kwa sababu kulikuwa mbugani wanyama pori  walikuwa wengi tena karibu . Walilinda wanyama pia zao la uyoga lilipatikana kwa wingi  kama vile;

Amanyansuka,  (b)   amanyageswa   (c)   Omwingira     (d) Amanyankobiti

Ibilogose

Mazao hayo yaliwapa mboga wakati wa mvua sehemu hiyo ya Guchindama  hakukaa sana kama sehemu zingine wakati huo tayari jamii ya wairege ilikuwa imekumilika kwa vizazi vine yaani ( amakora). Kwa maana amakora yalianzishwa huko Magongo. Jamii ya Mwirege iliyoondoka kutoka Magongo walikuwa jamii kubwa sana kwa maana wao walihesabu miaka kwa njia ya vizazi yaani amakora. Kila kizazi kimoja kikabaki kimoja kwa magango walieli takribani miaka 200 tangu walipotoka Kondoa.

Kwa hiyo kizazi kiliechofia Mogango ni ABASAE na ABAMAIRABE ambao ndio wa kwanza kupewa jina hilo. Waarabu na Wasae wao walizaa wagini na Wanyambuli vizazi hivyo vilipata unabii wa kwenda getasengeri.

SAFARI YA KWENDA GETASENGERI:-

Nyairo ambaye alioa wake wanne ambao ni

(1) gasembe   (2) Mosoba   (3) Malale   (4) Nyamwamu

Jamii za watu hao zilikuwa kubwa ambazo ziliingia nchi mpya ya gelasengeni. Watu walitoka Guchindama ni

Siye alimzaa Obago.   Obogo alimzaa Mgini.  Mgini alimzaa Tugara na Mwera.

Maili alimzaa Wangeze. Wangeze alimzaa Gasaya. Gasaya alimzaa Chacha.

Gibecha alimzaa Telili na Marcoo . Teleli alimzaa Muko na Muko na Moryoo alimzaa Matiko. Kihore na Mohere alimzaa Manga. Hiyo ndiyo jamii ya gibecha.

Nyakiguchi malio ndugu zake ambao ni  wambura Sagire kimwana na wake zao.

Giichere na familia yake wote waliondoka kwenda nchi mpya ya Getasengeri wakati huo aliyekuwa kiongozi mkuu wa msafara ni Mwita habuba. Yeye alikuwa mzaliwa mila ya wairege ( Mchama) tena wakati huo wairege walikuwa marafiki na wamasai yaani (abackwel) na jamii nyingine za wagusuli wate waliondoka kwenda gelasengeri

KUINGIA NCHI YA GETASANGERI

Waliondoka kutoka guchindama kuelekea Getasengeri ambapo waliingia huko wakiwa pamoja na wakaii yaani wagusui lakini zao zingine hazikwenda pamoja nao ila zilikwenda upande wa magharibi. Walipofika huko walifurahi kupata nchi nzuri yenye rutuba nzuri ya kulima,wakaanza shughuli zao za kulima na ufugaji. Walilima mtama na ulezi na viazi. Mtama waliolima ni (EKOMBA) na ulezi walilima Isabara Cegeseyekwe)  karuma viazi walilima (Nyagasinda)   tayari wakati wangari wageni huko. Kulitokea ugomvi  baina yao na wagusui ambao ulisababisha kutengana. Kwa

hiyo wagusli walijitenga kabisa


wakahamia sehemu moja inayoitwa (Ngabone) wakakaa huko lako. Lakini wairege walibaki kule getasengori ambapo hapo  ndipo walipookaa wairege. Wairege walifanya kazi zao za kufuga na kulima walipolima wakapata mazao mengi ya chakula na mifugo ikaendelea vizuri kwa mara ya kwaznza bila ya kuungana na jamii zingine za kikurya ambazo walishirikiana hapo awali wakatahirisha tohara ambayo iliwafanya wajisikie kuongezeka kwa saali walipomaliza shughuli ya tohara tayari wakapata nguvu ya seeli wala wazee waliotoka mogango na Gunchindama tayari nao wakandaa sherehe ya Jublee yaani ISUBO. Wakasuba wagini kwa mara ya kwanza.

Kwa hiyo kundi liliongozwa na MWITA HABUBA ambaye ndiye aliyeleta shughuli hiyo wa kwanza kabisa huko Getasengeri. Wakafanya hiyo shughulli ikamalizika salama. Ikawa historia nzuri kwa wairege. Kwa hiyo jamii yote ikasema amina. Maana lilikuwa jambo jema kwao tangia wakati huo wairege wakawa na wazee wanaoitwa (Wasubi) ambao ndio walikuwa waamuzi wa mwisho kama kuna jambo gumu. Kwa hiyo wale wazee wakawa tayari kutoa maamuzi ambayo hakuna mtu mwingine atapinga. Ikawa hivyo Getasengeri ni sehemu ambayo wairege walianzia tamaduni nyingi ambazo zipo mpaka leo. Sheria ya jamii miiko, ibada matambiko, harusi sherehe kutoga masiko, kutoa meno ya mbele (inyenya) ( Bibisaku kumi na mbili  (12) tohara za wangineamang’ara0 abanchongwe abangicharu. Hizi ndizo tohara za kwanza

wairege walipoingia  huko Getasegeri sherehe zilizo anzishwa huko ni kama vile’   Isubo,  Ndoa ya mila )embagorya), Isaiga – lika, Kutoga masiko) obotora mantari),  Esaro -  tohara.

Kwa karne nyingi zilizopata jamii hiyo ilikuwa haitaki kulaumiwa na jamii  yeyote zilizokuwa jirani. Wairege walipenda kukaa upande wa mashariki kwa sababu wao walikuwa wakulima na wafugaji. Zama hizo za kale ya miliki hiyo iliandaa demokrasia ya utawala wa kijadi yaani (Kimila) kilichoongozwa na wazee waamue bisara ma jelo,a tema wemue fa,o;oa zomzpemde;ea.

KUPATIKANA MILANO 12 YA WAIREGE (IBISARU)

Jamii hiyo ya wairege tangu  kuzaliwa zimepita takribani karne 8½  sawa na miaka 860 hadi 2014. Huko Mogango mtu huyo alizaliwa mtoto wa pekee bila kuwa na ndugu yake alikuwa mwana pekee wa Gurani na gurani alizaliwa na mkury na mkurya alizaliwa na Mogango omanto. Mwirege alijaliwa  kuoa mke jina lake aliitwa

Nyamokara) aliyemwoa kwa wagusuli. Mama huyo wa wairege alijaliwa kupata watoto wawili wa kwanza aliitwa Nyairo na wa pili aliitwa Nyasunjye. Vijana hao wawili ndio

waliozaa jamii yote ya wairege ambapo taifa la Tanzania linaitambua kwa mchango mkubwa wa kimaendeleo.

Kwa hiyo tangu mwirege hadi uhamisho wa Getasengeri ni karne mbili sawa na miaka (200)   kwa hiyo wairege walihamia Getasengari kali  hadi mwaka 1360 – 64 Unabii unaonyesha wazi kuwa vizazi amakora yaliyopita ni nyakati walizoishi na tangu uhamisho huohadi Ibisaku ABAKEHENJE NA ABARISENYE) vizazi(2) na tangu abalisenye na abakeherye monyomala molacha – sherehe ya wairege kujiita

engwe ni karne mbili yaani vizazi hadi uhamisho wa bilali kwa hiyo wuhamisho wa bilila unabii unaonyewsha kuwa waliohamia bilila ilikuwa 1760 – 1764.

Na tangu uhamisho wa bilila mpaka unabii wa Samaya na mwzsi kwenda Somoche na mchanjara yaani nyamuaga hadi 2014 ni zaidi ya miaka 250. Kwa hiyo tangu mwirege

hadi 2014 ni zaidi ya miaka (850) mia nane hamsini iliyopota. Kwa hiyo wairege wanajulikana kwa majina mawili yaani ENSEMBE na WAHAIBARA).

Hayo ni majina mama ya wairege hata kabla ya )egwe)

(1)  MBANYAMISAMU ABATISINI ABANYAKIGUCHI KENG’EMBE

Mlango huu umezaliwa na mama jina lake nyawamu aliyeokotwa na Nyairo Mwirege. Akiwa na watoto wawili wakwanza alikuwa na begi ambayo ni 9Iliguchi) na wa pili alikuwa na ngozi ya ng’ombe yaani (Iluho). Nyairo alimchukua akamfanya mke wake baada ya hapo alijaliwa kupata watoto wengine ambao ni:-

Sagire , Kimwama, Wambura, Lawe.

Basi mlango huo uliendelea vijana wote walijaliwa kuoa wake kila mtu na kaya yake.Sagire alimzaa wambura,  rimwana alimzaa mwita,  Mako alimzaa Merama, Lowe alimzaa Mniko.Kwa hiyo mlango huu una kaya sita yaqani (AMAGIHA) ambayo wenye neema kubwa kati ya milango (12) ya wairege. Kupitia mzee wa Mniko awe ambaye aliwatengenezea. Baraka kubwa wakati wa wantinguti abaruga mabele na magula na nyama ya Bhoke huko bibila kwa kuwa mzee huyu alitajirika utajiri mwingi wa ng’ombe na mbuzi na kondoo kwa hio  nao wana kaya sita yaani ( amaghina)(a) Abahiri chacha,  (b) Abahiri   Lae,   (c) abahili   Maho    (d) Abahili   Merama,   (e) Abahili   Mwita Kimwana,   (f) m abanyamwamu   abanyamalosi, (g) Abanyakiguchi.Hizo ndizo kaya za mlango wa anyamwamu mniko lawe alimzaa maniko. Maniko alimzaa Chacha maniko. Chacha alimzaa Mwita chacha ambaye ndiye milionea wa kwanza wa kige. Kwa barka kwenye mlango uo ni sana tena wanyama walipata dhumuni ya utajiri wa watu na mali. Mtu  huyo ambaye aliitwa Mniko Lawe yeye alizaa vijana wawili ambao ni Manko na lawe. Lawe alimzaa Bhoke. Bhoke alimzaa Magari na Chacha na Muniko alizaa chacha – chacha alimzaa Mwita Nyambuna ambaye ndiye milionea wa kwanza kwa wairege. Saiga yake ni ABANGINEI ya mwaka

1946-50.

(2). ABAHILI OBOGO PA NGOMBE:-

Nyairo alioa mke jina lake aliitwa Gasembe. Gasembe aliolewa kutoka kwa Isanye baka ambaye alimzaa Siye. Siye alimzaa Obogoso alimzaa Mera tagare kemogo tagare taiigwa gichogo na Nyakiguna. Mlango huu wa Oboga ni mkubwa kati ya milango 12 ya wana wa wairege. Vijana wa Obogo wa Obogo nao walijaliwa sana neema hasa wakati wa miiko ya kirege ambayo watoto wa

Obogo walikataa kutii ndiyo maana upande wa hizi mlango uliongoza katika zama hizo za kale.

Basi abogo alijaliwa kupata kijana jina lake Mgini ambaye alitambikia wakati wa samaye na mwasi walipotoa unabii. Kuhusu vita dhidi ya wamasi. Kwa hiyo, unabii wa mwasi alipoleta kwa jamii mgini alichukua kwa hiyo baada ya

kuanza vita vya wamasai huko bilila kundi la samaya lilienda somoehe lakini huko wamasai waliwafuata kuwaua. Ndipo kundi la mwasi lililoenda mchojara yaani yamwago lilipata taarifa kwamba ndugu zao walioenda Ssomoehe wameuwawa na wamasai basi magini omwinga akapanda mlimani na kufanya tambiko akawasha moto kila siku wale waliyonusurika  wakaona naowakawasha moto

huko Ikorongo. Kukawa na ishara ya kutambuana kama ndugu kwa hiyo mgini alimzaa Moseli. Moseli chacha na Kchongo na Obogo. Mlango huo ndio wenye jamii kubwa kuliko yote ya wairege una magoha mengi yenye watu mashuhuri.

Majina hayo ni:  a). Abanyakomoga   (b), Abahiri  Tagare   (c) Abahirij Mwora

    (d) abahiri Toigwe   (e) Abahiri  Gehogo   (f) Abahiri Gohago

(g) Abanyakiguna.

Wahiribogo ni mlango wenye sifa kubwa ya utafutaji wa mali una asili ya utajiri hasa katika karne zilizopita . Lakini katika karne ya sayansi na teknorojia wamepata K

Umaarufu sana. Basi kwenye kaya ya Nyakemoga ambyo katika mlango huo kupitia uzao wake walioubogo una majivuno sana kwa sababu Nyakemoga  alimzaa Bhoke. Bhoke aimzaa Mwara na chacha kwa kuwapata watu hao tumepata faidakubwa ambapo mlango huo ndio wa kwanza Tanzania . Nyerere ambaye mama yake ametoka katika mlango huo. Tena kupitia wahiliboga wairege wamepata Mbunge wa kwanza kutoka kwa wairege ambapo tangu Tanzania ipate uhuru watawala walitoka sehemu zingine za wakurya lakini si za wairege. Kwa hiyo mbuge wa kwanza kutoka kwa wairege ametoka kwa wahirioboga. Kwa hiyo mbuge wa kwanza kutoka kwa wairege ametoka kwa wahiriboga ambaye ni mhe. Charles Mera nyanguru. ( Umnyakemoga) tena mlango ;umekuwa wa kwanza kimqaendelei kwa kuzaa watu wenye sifa na maendeleo .

Kwa hiyo wairege tangu enzi za mababu hadi (2074)  mlango unatawala kiuchumipamoja na wahirioboga ambao kupitia uzao wao tumepata utajiri BILIONE HII WILISONI KIGUHA ) Umunyakomoga.

3). ABAILI NGEZE;-

Nyairi alioa mwanamke jina lake Gasembe aliyemzaa maili na maili alimzaa Wangeze Wangeze alioa mwanamke jina lke bhoke Osimbori ambaye alimzaa gosaya na Mwinga.  Gisaya alimzaa Chacha na Mwiga alimzaa mwita. Kaika zama za kale mlango huu ulikuwa na asili ya siasa na kupitia kwao tulipata

watawala kabla ya mkoloni huku Nyamwogo ambapo watawala walitoka kwenye mlango huo walikuwa wawili ambao ni.

Mhe. SERYA GASAYA- Omokama) mwenye hukumu ya mwisho

Mhe. CHACHA MGWAWA – Omokama vile baada ya Serya kwa hiyo huo mlango una asili ya siasa tena mlango huu ndio ullleta hasara ya kuchoma shule ya Bunginre chanzo ni utawala na watu waliochoma ch shule hiyo walikuwa wanatak kumwondoa chogo kwenye uongozi . Mlango huo ulikuwa maarufu kwa kupiga

\

4).    ABAHILI MANGA:-

Manga Omohere  Ogibeche Omita Onyaibara Nyairo Omwirege alioa mwanamke jina lake Mosoba kutoka kwa wanyaibara aliyezaa Mwita kw. Kwa hiyo Gibeche ndugu yake alikuwa Moryoo ambaye alimzaa Matiko. Kwa hiyo  

Mosoba alijaliwa kuzaa jamii iliyoitwa (Monyo mahe monyomahe niro walitoka milango sita ambayo ni;

(a) abahili manga   (b), Abahili Matiko,   (c) Abaleleli,   (d) Abahili kehore(e) Abanyangab

Ambapo Mosoba alimzaa Mwita Nyairo na alimzaa habiba. Habiba alimzaa Mwita ahababa Gibche kehore na moryoo na Mchore Baadae Mohere alimzaa Manga huko Getasengeri Mlango ulioa wanawake kumi na mbili wakati wairege walitka Getasegeri na kuingia Gairoro na mnyunyi Gutaro na igena itambe mango ndio alikuwa kiongozi mzee wa (mchama) tena mango amahore ndiye aliyewafukza wanyamongo kutoka bilila wakatiwake na siraye tena aliwafukuza wasweta toka mchonchara – yaani (Nyamwanga)

Yeye aliandaliwa sherehe na jiroyemnyamongo huko bilila alikwisha kusherekea akasema wewe Siraye ingelijua kama hiyo sherehe  ningekuja kube hauna vitu kabisa jiraye iliposikia hao maneno ;ya manga kwa hasira alimwambia wewe haufai sisi sote ni ( wanachama) viongozi kama wewe ni mwema umeenenda wanche joelina mimi niandae jeshi kasha tukutane kaama atkayechuda mwengine manga aliposikia hayo maneno alicheka naye akajibu upange sehemu ya kukutanishia jeshi , wakapanga Tagare.

Basi manga aliporudi kwao, aliaandaa jeshi lake vizuri lakini siku ya vita kulikuwa vituko manga aliwachukia wake wake akawapa manyoya ya mbuni

chinsangari na mkuki na ngao wakavaa vichwani kwa maana hayo manyoya hayakuhusia kwa mwanamke. Lakini manga yeye aliwavalisha jeshi lake la kike. Basi likatangulia vitani baadae wakaja wanaume jeshi la kiraye lilipoona hayo likashangaa wakati wanashangaa wingi wa jeshi kumbe askari wengine wa manga wamezungukia sehemu nyingine kwenda kuchoma nyumba wanyamonga.

Basi manga akamshinda kiroya kwa hiyo manga ndiye aliwafukuza nyamanga kutoka bilila tangu wakati huo hadi leo wanyamongo walihama jumla kwenda nyamongo na katika historia ya ushirikiano tena wengi walimalizana kwa ushirikiano. Kwa hiyo wakati wairege wanaingia Gairoro Gutura Muyiyi walimanga ndio walikuwa kiongozi yaani (inchama) huyu mangoa alioa wake wengi ili awe na familia kubwa lakini hakujaliwa watoto. Lakini kwa upande wa vita wakiweka historia ya kuwaondoa

wanyamango ambao mwanzoni walikuwa walacha walivimanga sio sana sifa yao kubwa ni wife mlango huu ambao umetoka ktaka sehemu ya wanyomale na upande wa wakchgenje.

5)   ABAHILI  MAZIKO:-

Matiko alizaliwa na Moryoo na Moryo alizaliwa  na Gibeche na ndugu yake Teleli. Basi Matiko  ndiye baba wa Matiko. Katika zama hizo Matiko alitenda tendo la kihistoria kwa jamii yeye alijaliwa kumpa mtoto wa manga ambaye manga alimzaa na magina alikuwa ndugu yake Matiko na matiko akampa mimba mwnae mtoto wa ndugu yak e baada ya tendo hilo la kihistoria ile aibu na huko kwa waruo aliofika kwao alifanywa mtumwa akakaa huku muda mrefu tangu ujana wke hadi uzee .

Basi aikiwa huko ndugu zake walifanya bidiii ya kumtafuta mwishowe walimmpata. Maa baada ya kupata taarifa kuwa Matiko yuko ujaruo jamii yao

ilienda huko kumsaka . Walipomkuta walilia kwa sababu ndugu yao aliyepotea wamempata. Basi wlaipomwana wakamwangukia wakasalimiana. Matiko akawaficha ili wenyeji wasiwaone. Lakini

ilipofika usiku, walichukua kilicho chao kwa kuwa Matiko alikuwa ameisha pata mke huko ujaruoni na ana watoto tena familia ilibidi waondoke nayo huo suku. Wakasafiri hadi kwao.  Basi  Matiko alipokuja ilibidi ahame kizazi kingine ambacho hakuwepo tangu awali akahamia moyo  mambo hayo yoate kuisha Matiko alikaa na familia yake hadi ikakamilika mlangowa waliwalimatiko. Basi aliporudi kwao alikuwa na wake watatu ila watoto hakuwa nao wengi.

Ndipo alimwoa mwanamke jina lake Matinde na wale wengine walikuwa ni ; (i) Wairanya   (ii)  Nyakareto   (iii)  Msweta.   

 

Laikini hao wanawake uzao wao ulikuwa wa shida. Basi baada ya kumwoa Matinde ile hali ya kuhesabu miaka ilikwisha akaendelea kusubiri ni siku gain matinde atapata mamba analau amwondolee aibu ya kuambiwa yeye wake zake hawakutehiriwa maana jamii aliyokuwa nayo iliitwa (Irinyinya) yaani watu

ambao hawakutahiriwa. Basi hali ikawa mbayazaidi . Siku moja alikasirika juu ya mke wake Matinde kwa kuwa hakuwa na mtoto akamfukuza kutoka kwake. Basi yule mama kwa majonzi alilia sana lakini kwa kuwa hana namna aliondoka kwenda kwa rafiki yake Matiko huko ngureme wakati akiwa njiani , faraja ikaja akashangaa kumwona mtoto njiani ambaye hana mtu wala msaada. Basi yule mama  kwa huruma akakichukua kile kichanga akatazama ni wa kiume ial safari ya kwenda ngureme iliishia njiani. Ikawa faraja na furaha akarudi akiwa na mtoto. Basi Matiko alipomwona akakuta ana mtoto akamuuliza maswali bali

alinyamaza kimya yule mtoto alipewa jina la MISIWA na baada ya Miiriani  kuwa mkubwa yule mama alilpata mamba uzeeni akamzaa mtoto jina lake Miam. Basi Matiko akapata bijana wa kiume wawili uzeeeni..

Basi Msiwa alijaliwakupata watoto wakwanza alikuwa ni:-

(i)  Matiko Misiwa,   (ii)   Nyangi Oseba   (iii)     Magori    (iv)  Magori  

(v) morroo

Basi Miriani alioa mke jina lake Mogesi ambaye alimzalia kijana jina lake Igaina Igai alimzaa Mariba na wambura. Basi hicho ndicho kizazi cha Matiko na upande wa kaya

( gmagiha) ni”

(i) Getera  abalili   (ii)  Abahili   nyangi  oseba    (iii)  Abalili  MataigaMlango huo nao walikuwa monyomahe.

6) ABANYANGABI NA ABAHIRI KEHO.RE:-

Wanyangapi wana historia nzuri kwanza kupatikana kwa jina la nyangabi . Huyu nyangabi alizaliwa na mama yake ila hakujua baba yake ni nanai?  Mama yake aliyempa mamba hakumtaja k amwe kuwa hiyo yeye ndiye alihangaika na mamba mkpaka akazaa. Basi alipozaa yule mtoto akawa na shida kwa maana wakati huo watu walikuwa kwenye zama za kutumia ngozi kama nguo. Sasa basi yule mama hana wa kumtengenezea nguo na ua atatoa wapi hiyo ngozi ndipo alienda  kisimani akamkuta mnyama aiitwaye Engapi yaani mbuzi mawe

akawaita watu wamchunie ile ngozi yake ili apate nguo ya kumfunika mwanawe. Hapo  ndipo jina la nyangapi lilianza hadi leo huyu mwanamke alikuwa msichana  wa Kehore. Jina lake aliitwa Gati. Kehore nyangapi akekuwa kwa maisha magumu akiwa kwa baba yake na mama yake hakupata mwanamke kamwe. Mpka kifo.

Basi huyo nyangapi alijaliwa kuwa na jamii kubwa ambayo ndiyo wanayangapaai yeye nyangapi alimzaa Kiruka. Kiruka mwita tena Mwita alimzaa Giscubiti tajiri wakati wa ubantingiri abaruga mohere na matuta Gisulilti alijaliwa utajiri mwingi ila yeye mwenyewe aliharibu. Kwa kumwaga maziwa kwenye mto bilila wakati wa mashindano ya utajiri wa ng’ombe na Mniko lawe Baadae Gisubili alimzaa wangwe na wangw alimzaa Kegoeha. Kigoha na Mwita nyaronyo – nyaronyo alimzaa Moseti. Basi hao ndio mababu wa wanyangapi tena wanyangapi wana sifa ya wume zao wakiolewa hawakuzaliwa Getasangari walizaliwa Garoro. Wakati wa vita vya kwanza ya

wairege na wamasai vita hivyo ndivyo viliwafannya wamasai kuhamia bilila kabal ya wairege. Lakini baada ya kutahiriwa siaga ya abangine amang’ara waliandaa jeshi la kuwaondoa wamasai kutoka bilila ambapo badae wairege walijitenga na walacha yaani wanyamongo wakahamia bilila hao ndio waliowaondoa wamasai kutoka bilila kwa kutumia shujaa wao aliyeitwa (Timbo) ambaye walimchoma mkuki lakini hakuumia. Kwa hiyo watu waliogopa sana. Lakini hao wanyangapi pamoja na wahirikehore waqlikuwa pamoja ndio maana wao waliwameaq wahirikihoreambao ndio baba za wanyangapi kwa wahirirehore. Waliwatoa sana hao wanyangapo walitengana baada ya wairege kuhamia nyamwaga naye Kihore akawa na jamii ndogo sana ambayo haina historia kubwa na baada ya wairege

kuhamia nyamwaga jamii yake Kihore walikuwa ni Guragura chacha Masiani na  bwiso kwa upande wa kaya kwa wanyangapi wana amajina haya;

(i) Abahiri Wangwe,       (ii)  Abahiri  Moseti    (iii)  Abahiri Kagocha..

Kwa upande wa wahirikehore wana kaya yaani amagiha

(i)   Abahiri Masiani,   (ii) Abahiri  Bwiso  9iii)  Abahiri  Guragura. Na jamii ilikuwa kwenye kundi la manyamahe tena baba yao alikuwa kchora alizaliwa na habuba baba yake na nyomahe mama yake ndugu walikuwa ni;

(i) Mwita  chabuba,   (ii)  Gibeche   Ohabuba.

Monyombihe baadae iliitwa wanyaroara tena baada ya kutoa muungano wa bisaku iliitwa abakehenje. Kwa wairege ukitoka wakuelewe harka sema ‘

(a)  ensombe na      (b)   Wanyaibara.

Ukisema hayo wairege wote utakuwa umeuguzqa kila mtu.

8). ABANGOHE PA MOCHE:-

Mango wenyo sifa kubwa sana kwa wairege kwa sababu ya kutulisha tangu wairege alipojitenga kutoka kwamuungano wa kutahiri pamojana majirani zao mlango huu wa wangone ndio wenye dhaana ;ya kutuhiri Mongohe alizaliwa na Malale na ndugu yake wankala baba yao ni Nyairo Omvirege. Nyairo alikuwa na wake  wane naye malae ni mmja kati ya wake wa nyairo alimuoa ktoka Butimbaru na na huyu malale baba yake aliitwa Sabayi. Basi Magohe alialimzaa

Marwa kwa jina la utani Mairo na Marwa . Marwa alimzaa Chacha. Chacha alimzaa Sabai Keremba Ogoma mosagaro. Basi hiyo jamii ikawa kutoka kwa watu wachache badae jamii kubwa mlango huo wa wangohe hawana sifa mbaya kama milango mingine kwa sababu wao kazi yao kubwa ilikuwa ya kutoa Gairoro gutura Mnyuyi hadi bilila. Jamii hiyo ndiyo ilikuwa na dhamana ya  kutahirisha hata walipokwenda Somache (Ikorongo). Kazi hiyo ya kutahiri kwao sio tatizo ni kipaji toka awali tena mlango huo una historia kubwa ya ng’ambo ambayo waliifanya kazi kubwa na nzuri kwa jamii ya wairege ng’ariba hao walikuwa ni:-

(i),  Mahando  (ii) Marwa   (iii)  Humtunyi  (iv)  Matiko Humtunyi. (iv) Marwa Chumtunyi

Hawa _______________________________kwnye mlango wa wangole tangu nyakati za bilila hadi kuhamia mchacharo yaani nyamwega.

Mahando – alifaniksha tohara za kwanza baada ya wairege kutokabilila na kuingia myamwaga. Kati ya mwaka 1850 wairege walipohamia mchacharo waliandaa tohara ambayo walitahilia vijana wao.

Baadae alimfuta marwa

Baadae tena hutunyi.

Na ngariba alijaliwa anaweza kutahiri tohara zaidi ya(100% kwa hiyo wangohe sifa yao ni kutahiri vijana kwa wairege.

8). ABAKIRUMBE:- BWOMMIRI INYA MUGAMBI

Abakilumbe ni mlango kati ya milango  (12) ya wairege ambao wamezaliwa na malabe aliyeolewa na nyairo Omirege kutoka kwa watimburu. Baada baada ya kuwazaa vijana wakubwa aliwazqaa Nyangwe. Nyangwe alimzaa Kirumbe ambaye ndiye aliyepanda nyama shambani. Mtu alikuwa mwana sayansi alijaribu kuweka historia kubwa lakini ile sayansi haikuwa na matokea mazuri. Baada ya ile mbegu kuoza lakini ingeota mngelitambua mchango wake kwa sayansi. Mtu huyo alitafiti sana maana ya kupunguza vita vya wanyama hapo alipochukua hatua ya kuchinja ng’ombe hiyo na kwenda kupanda shambani , kusudi lake lilikuwa la kufikiria mbali. Lakini nyama ile ilioza haikuota. Basi kirumbe alimzaa Samuye nabii ambaye yeye alitoa unabii wa wairege kwenda somoche ingawa watu waliokula unabii wake walienda huko Samache walikufa sana wakati wa vita na wamasi wakirumbe wana sifa nzuri tangu wankoba hadi samuya. Wakirumbe ni koo yenye kupendwa sana na koo zingine tena mabinti wao walikuwa wamegombolewa na vijana wa koo zingine

kwa sababu ya upole ni uzao wa wankaba aliyemzaa nyangwe. Nyangwe amemzaa Kirumbe – Samoya na Makoro tena wana kaya amagilia

abahiri wankaba

Abanyamatong’ana

Abahiri kichongoro

9).  ABASESE ABATUKI PAROKO

Mlango huu wa wadese baba yao ni mmasai ambaye alioa binti wa Kirege aliyekuwa mtoto wa Gichore Omwirege. Binti huyo baada ya kuolewa kwenda kwa wamasai alipata misuko suko mingi kwa sababu alipozaa watoto wake wengi walikuffa hata mme wake akamchoka jina la mume wake aliitwa (MRUMBASI) . masai huyo, alishangaa sana kwa matatizo hayo ya kufiwa na watoto. Lakini baada ya muda mrefu kulitokea njaa kwa wamasai. Wakati kulitokea janga hiloo la njaa huyu mke wa mrumbusi alikuwa na ujauzito. Njaa ilipoendelea ilibiri arudi kwao kwa wairege huko Gitasongori. Yule mama alipokuwa njiani anarudi kwao, alijifungulia njiani mtoto wa kiume. Kwa kuwa yule mama alikuwa amefiwa sana na watoto alipompata yule mtoto alikuwa

amechoka akampepea ili apate nguvu yaani alisesa yule mtoto mwishowe warifika kwa wairege ndipo wasese akatabiri pa rook aberumbasi pa Gimonge.

Basi yule mama alikaa kwa baba na mama yake tena hakurudi tena kwa wamasai hadi leo. Basi msese alikuwa mkubwa hadi kaoa na baada ya kuoa alimzaa mtoto jina lake Mahucha na Mahucha alimzaa Gimang’anya. Basi Gimang’anya alimzaa (Gimonge0 ( Isare) na ( Kemege). Basi kaya ndiko ametokea Eliya mwenye nguvu mtu hodari wa vitu aliyeitwa wairanga huyu

wairanga ndiye aliyewauwa wamasai wakati wa wairege waliitwa na wamasai  kwa jina la (nkari  chaito) yaani wake wao ilikuwa dharau kubwa kwa wairege kuitwa jina hilo  ingawa hawakuwa na nguvu za kuwapiga wamasai. Wamasai walikuwa na jeshi lenye nguvu laikini kipindi cha huyo shjaa wairege alijitoa mhanga kwenda kwenye kituo cha sai yaani kwenye jiwe la balitilo lilipo Geisangora.

Wakiwa na rafiki yake jina aliitwa Mwita Msereta mnyamwamu kwenda sehemu ya vita wao ndio waliwaona wamasai ambapo wamasai walikimbilia laliondo na masai mara kwa hiyo wairenge ni shujaa alikwaokoa wairege kuoka kwenye cotonila wamasai. Siku  masai walipouwawa. Huyo wairenge alikuwa na sherehe numbani kwake na waiarenge alizaliwa na  Mwita ambaye alizaliwa na Isare. Mlango huo watu waliwaita wamasai kwa jina la abasese abalori gimung’aya abarimbazi baGimonge abaatori paroko. Mbale gucha pa lamunya tene mlango huo milango mingi hawakuoa mabinti wao isipokuwa wangohe na wahiringeze ndio walikuwa wanapenda kuoa kwa wasese lakini mlango huo ulijaliwa kuwa na mabinti wazuri sana.

Content Disclaimer

Informasi ini disarikan dari Wikipedia dan disajikan kembali untuk tujuan edukasi. Konten tersedia di bawah lisensi CC BY-SA 3.0. Kami tidak bertanggung jawab atas ketidakakuratan data yang bersumber dari kontribusi publik tersebut.

  1. The information displayed on this website is sourced in part or in whole from Wikipedia and has been adapted for the purpose of restating it. We strive to provide accurate and relevant information, however:
  2. There is no guarantee of absolute accuracy. Wikipedia is an open, collaborative project that can be edited by anyone, so information is subject to change.
  3. It is not intended to constitute professional advice. The content displayed is for informational and educational purposes only. For important decisions (e.g., medical, legal, or financial), please consult a professional.
  4. Content copyright. Wikipedia is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike License (CC BY-SA). This means that content may be reused with appropriate attribution and shared under a similar license.
  5. Responsible use. Any risk arising from the use of information from this website is entirely the responsibility of the user.